Mkutano Mkuu TAPSEA,TRAMA kufanyika Mei 2023
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa utakao wa husisha makatibu mahsusi na watunza kumbukumbu wa sekta ya umma na sekta binafsi Tanzania unatarajiwa kufanyika hapa zanzibar mwezi mei mwaka huu.
Waziri Nchi Menegment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe, Jenista Joakim Mhagama ametoa tamko hilo wakati akizungumza na watendaji wa wakuu wa Afisi ya rais kaiba sheria utumishi na utawala bora ,Makatibu mahsusi (TAPSEA) na chama cha watunza kumbukumbu Tanzania (TRAMPA
Wakati akielezea dhamira ya serikali ya juu ya kufanyika mkutano huo hapa visiwani wenye lengo la kuwajengea uwezo watendaji hao ili kuhakikisha wanatekeleza kazi zao,kwa ufanisi na kwa usiri, mkubwa katika serikali zote mbili.
Amesisitiza kuwa kada hizi mbili ni kada muhimu za kuhakikisha shughuli za Serikali zinaenda vizuri na Sekta binafsi zinafanikiwa na kuleta tija na taifa kwa ujumla.
Waziri mhagama alibainisha kuwa mkutano huo wa siku tano utaambatana na mafunzo kwa watendaji hao kwa ajili ya kuimarisha utendaji wa majukumu yao ya kila siku.
Akizungumza katika kikao hicho Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Katiba sheria Utumishi na Utawala Bora,nd Omar Haji Gora amesema lengo la kikao hicho ni kuangalia naamna bora ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan la kufanya kikao baina ya watendaji wa pande zote mbili za muungano.
Mwenyekiti wa chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania nd,Zuhura Songambele Maganga ameeleza kufarijika na agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwani linalenga kuwaunganisha na kufanyakazi kwa pamoja kwa maslah ya nchi .
Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Watunza Kumbukubu Tanzania nd.Devota George Mrope amesema wanashukuru ushikiano wanaoupata kutoka Serikalini , wataendelea kuwa mabalozi wazuri na kuendelea kutunza na siri za Serikali.
Wakati akizungumza katika mkuutano mkuu wa chama chawatunza kumbukumbu Tanzania (TRAMPA) Arusha, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania alitoa agizo la kufanyika kwa mkutano huo wa pamoja Zanzibar