Govt. Logo

OFISI YA RAIS - KATIBA SHERIA UTUMISHI NA UTAWALA BORA

Govt. Logo

Tathmini ya upimaji na utendaji kazi kwa watumishi wa umma

news phpto

Tathmini ya upimaji na utendaji kazi kwa watumishi wa umma

Watendaji na Viongozi wa( OR )Utumishi wa Umma na Utawala bora wametakiwa kuhakikisha masuala ya upimaji na utendaji kazi kwa watumishi wa umma yanafanywa kwa umakini na uadilifu.

Aliyasema hayo Katibu Mkuu (OR) Utumishi wa Umma na Utawala bora Yakout Hassan Yakout wakati akifungua mafunzo hayo ya tathmini ya upimaji na utendaji kazi wa watumishi wa umma huko ofisi kwake mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Alisema endapo ukiwepo umakini na uadilifu katika kumpima mtumishi kasoro ndogo ndogo zitaweza kuondoka katika masuala hayo,na kufanya utendaji wa kazi kuwa rahisi kwa viongozi na watendaji.

Nae mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka (OR)Utumishi wa Umma na Utawala Bora Maulid shaib wakati akitoa mada hiyo ya tathmini ya upimaji na utendaji kazi kwa watumishi wa umma amesema upimaji kazi ni kitendo cha kumfanyia tathmini mtumishi majukumu yake ,kwa kipindi kilichopangwa ili kuweza kufikia dira na malengo yaliyokusudiwa.

Alisema katika upimaji huo ni lazima kuwepo na makubaliano ambayo yana nyenzo muhimu ya kukuza utekelezaji bora majukumu kulingana na kada husika.

Nao baadhi ya washiriki wakichangia mada wamesisitiza kuwa fomu ya makubaliano ni ya pamoja na msingi wakupata muafaka uliweokwa hivyo basi, kila mtumishi apewe nyongeza kwa mujibu atakavofanyakazi pamoja na majukumu yake aliyopangiwa Mafunzo hayo ya siku moja yaliandaliwa na ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar.

Contacts

Main Office
P.O.Box 3356
Zanzibar, Tanzania
Tel.: +255 024 2230038
Fax: +255 024 2230027
Webmail: info@utumishismz.go.tz
Website: www.utumishismz.go.tz
Pemba Office
P.O.Box 112
Chake chake, Pemba
Tel.: +255 024 2452294
Fax: +255 024 2452291

Us

Home About Us Departments

External Links

IPA OCAG ZAECA EGOZ MUFTI