Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi yatataka wakuu wa Taasisi kuhakikisha wanasimamia haki na wajibu kwa wananchi .
Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Machano Othman Said amewataka wakuu wa Taasisi kuhakikisha wanasimamia haki na wajibu kwa wananchi .
Ameyaeleza hayo wakati kamati walipokuwa wakisikiliza taarifa ya utekelezaji ya ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora huko ofisini kwao Mazizini .
Alisema endapo Ofisi hiyo ikisimamia haki na uadilifu ndani yake maadili kwa viongozi yataimarika,nidhamu kwa watumishi zitaongezeka pamoja na kuinua maendeleo ya taifa nauchumi kwa ujumla .
Alisisitiza kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ili kuweza kumsaidia mhe rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi katika suala zima la masuala ya utawala bora.
Nao baadhi ya wajumbe wa baraza la wakati wakichangia wamesema suala la udhalilishaji bado linachangamoto kubwa hivyo watoaji wa haki waangalie kabla ya kutoa maamuzi kwani bado wananchi wanapata usumbufu.
Aidha walisema suala la misikiti nalo lina migogoro isiyoridhisha na kushauri Ofisi ya Mufti kufanya biidi ya kutoa elimu za ndoa ili talaka ziweze kupungua mijini na vijijini.
Mapema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman amesema malengo na mikakati ya mwaka 2022/2023 ni kuimarisha upatikanaji wa haki na utawala wa sheria ,kusikiliza kesi na kutoa maamuzi ya haraka na kwa wakati pamoja na kusimamia utekelezaji wa mpango wa rasilimali watu wa mwaka 2022/2023.
Vilevile alisema kuimarisha matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika shuhuli za utoaji wa huduma za serikali pamoja na misingi ya utawala bora.