SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

OFISI YA RAIS KATIBA, SHERIA, UTUMISHI NA UTAWALA BORA

Sisi ni Nani


Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.

Mara baada ya Serikaliya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya 8 kuingia madarakani mnamo tarehe 3 Novemba 2020 hatua mbalimbali zilichukuliwa ili kuwezesha utekelezaji mzuri wa majukumu ya Serikali, kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu namba 42 (1), Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na Dira ya Maendeleo ya 2020. Miongoni mwa hatua hizo zilizochukuliwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Wizara 16 za kisekta ikiwemo Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa ajili ya kuandaa na kusimamia Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kuweka misingi imara na endelevu katika kuharakisha utoaji wa huduma bora na zenye tija kwa wananchi na kukuza maendeleo ya Taifa.

Baada ya Uchaguzi wa mwaka 2015 Serikali iliunda Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-KSUUB), Ofisi hii ilikuwa na jukumu la kusimamia Utawala Bora, kusimamia mhimili wa Mahkama, kusimamia shughuli za uendeshaji wa Mashtaka, Sheria, Utunzaji, Uhifadhi na Utumiaji wa Nyaraka na kumbukumbu, kusimamia Serikali Mtandao na kushughulikia Ofisi ya Hakimiliki. Lengo kuu la kuundwa OR-KSUUB ni kuwa na jamii ya kidemokrasia kwa kuzingatia misingi ya Utumishi wa Umma, Utawala Bora na haki za Binaadam.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliunda upya Ofisi ya Rais – Utumishi wa Umma na Utawala Bora mnamo mwezi wa April, mwaka 2019 ikiwa kwa ajili ya kusimamia, kuimarisha na kukuza masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar. Mara baada ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya 8 kuingia madarakani mnamo tarehe 5 Novemba 2020 hatua mbalimbali zilichukuliwa ili kuwezesha utekelezaji mzuri wa majukumu ya Serikali kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025 na Dira ya Maendeleo ya 2050.

Miongoni mwa hatua hizo zilizochukuliwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora kwa madhumuni ya Kuwa na Jamii inayoheshimu Misingi ya Utumishi, Haki, Usawa,Sheria, na Utawala Bora kwa Kuimarisha maendeleo ya Utumishi wa Umma, Kuweka Misingi ya Usawa, Sheria, upatikanaji wa Haki, kwa kuzingatia Utawala Bora ili kuweza kufikia lengo la Kuimarisha utendaji kazi katika Utumishi wa umma, kuratibu masuala ya Katiba, Sheria, na Utawala Bora na mahusiano ya kikanda na kimataifa.

  • DIRA
    • Kuwa na Jamii inayoheshimu Misingi ya Utumishi, Haki, Usawa, Sheria na Utawala Bora.
  • DHAMIRA
    • Kuimarisha maendeleo ya Utumishi wa Umma, Kuweka Misingi ya Usawa, Sheria, upatikanaji wa Haki, kwa kuzingatia Utawala Bora.
  • LENGO
    • Kuimarisha utendaji kazi katika Utumishi wa umma, kuratibu masuala ya Katiba, Sheria, na Utawala Bora na mahusiano ya kikanda na kimataifa.

VYEO, SIFA, MAMLAKA YA UTEUZI NA MASLAHI YA VIONGOZI KATIKA MUUNDO WA OFISI YA RAIS KATIBA SHERIA UTUMISHI NA UTAWALA BORA

Kuhusu Vyeo, Sifa, Mamlaka ya Uteuzi wa Viongozi wa Ofisi ya Rais- Katiba Sheria. Utumishi na Utawala Bora itakuwa kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Miongozo mbali mbali inayotumika katika Utumishi wa Umma.
Aidha, kuhusu Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Divisheni watateuliwa na Katibu Mkuu kufuatia mapendekezo ya Wakurugenzi wa Idara. Sifa ya kuteuliwa kwao ni kupendekezwa kwa mtumishi mwenye uzoefu wa kazi wa angalau Daraja la Afisa Mwandamizi katika kada inayohusiana na majukumu ya kitengo au divisheni husika.
Mishahara na Maslahi ya Viongozi wote wanaopendekezwa katika muundo yatakuwa kwa mujibu wa matoleo na miongozo kutoka Serikalini.