Mwalim Haroun alI Suleiman akutana wafayakazi wa Ofisi ya Mufti pamoja  na wa Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar

news phpto

Kutoka kitengo cha habari

Waziri wanchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala bora Mhe Haroun Ali Suleiman amewataka maulamaa na wafanyakazi wa Ofisi ya mufti kuendelea kutoa elimu kwa jamii kwani ndio msingi mkuu utakao wasaidia wananchi .

Kauli hiyo ameitoa wakati akisikiliza taarifa ya utekelezaji katika ofisi ya mufti huko mazizini.

Alisema maulama ni vyema kutoa elimu kubwa katika wilaya zote ili kuweza kuielimisha jamii na kupunguza utoaji wa talaka zinazotolewa kiholela .

Aidha aliwaahidi wafanyakazi kuzitatua changamoto zao na kuiomba Ofisi ya mufti kushirikiana na chuo cha kiislam katika kuhakikisha elimu ya kiislamu inaendeleakutolewa kwa ufasaha zaidi

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa ofisi ya mufti katibu wa mufti Nd.Khalid Mfaume alisema ofisi imejipanga kuendeleza utekelezaji wa shughuli zake li kutimiza lengo la kutoa fatwa ,miongozo ya kidini ,kuratibu na kusimamia shughuli za kiislam kwa kuimarisha utoaji wa fatwa ,tafiti na utatuzi wa migogoro pamoja na kuimarisha maadili mema kwa kupitia vyombo vya habari.

Wakati huohuo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman amesema wafanyakazi wa serikali mtandao wamepewa jukumu kubwa la kusimamia na kuhakikisha mifumo ya serikali wanaisimamia ipasavyo

Alisema hayo wakati alipozungumza na viongozi na wafanyakazi wa wakala wa serikali mtandao huko Mazizini

Wazro Haroun Hakuacha kusisitiza suala zima la kusimamia kwa umakini mifumo kwani sasa kumekuwa na watu wanaopenda kuingilia Mifumo ili kuweza kupoteza malengo ya serikali na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto walizonazo.

Mkurugenzi Utawala wa wakala wa serikali mtandao Nd. Khamis Mtumwa Ali Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya wakala wa serikali mtandao alisema kwa kushirikiana na taasisi mbali mbali za umma taasisi hiyo imeimarisha utendaji wa utoaji na upatikanaji wa huduma za serikali kwa wananchi na kupunguza mianya ya uvujaji wa mapato ya serikali kwa wananchi na kuanzisha na kutumiwa kwa mifumo mbalimbali ikiwemo mfumo wa ukusanyaji mapato ya serikali (zan malipo),mfumo wa ofisi mtandao (e-Office),mfumo wa ununuzi (e-Proz)na mfumo wa Bajet na Matumizi ya Serikalini (BAMAS).

Close
Close