Waziri Hroun awataka watendaji kufanyakazi kwa uwajibikaji na uadilifu

news phpto

kitengo cha habari

Waziri wanchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman amewataka watendaji kufanyakazi kwa uwajibikaji na uadilifu ili kuhakikisha utendaji wa kazi unaimarika katika taasisi zao.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati alipotembelea Mahakama Kuu na Chuo cha Utawala wa Umma(IPA) Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja kwa nyakati tofauti.

Alisema endapo kutakuwepo na utendaji wa kazi imara changamoto ndogondogo zinaweza kuondoka na kutatuliwa kwa haraka.

Wazir Haroun alisisitiza Viongozi kuondoa Urasimu katika sehemu za kazi ili kuweza kwenda sambamba na mabadiliko yaliyopo ya sayansi na Teknolojia nchini.

Mapema Mtendaji Mkuu wa Mahkama nd. Kai Bashir Mbarouk akisoma taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mahkama amesema Hadi sasa watumishi wa kada tofauti wameongezeka katika utumishi wa mahkama na kuondosha upungufu uliokuwepo ambao ulikuwa changamoto katika kufikia ufanisi ndani kazi.

Vile vile alisema baada ya kukamilika kwa jengo jipya la mahkama kuu na kuanza kazi kutumika, mradi wa ujenzi wa majengo mengine kumi na moja unatarajiwa kuanza kabla ya kumalizika mwaka huu.

Nae Mkuu wa Chuo cha Utawala wa Umma(IPA ) Dk Shaaban Mwinchum Suleiman amesema mafanikio ya chuo ni kuidhinishwa kwa muundo wa chuo, kurekebishwa kwa sheria ya chuo pamoja na kunzishwa kwa mifumo ya matokeo kwa wanafunzi ya oneline pamoja na udahili na kuendelea kuimarika kwa mafunzo ya kuwajengea uwezo , hakuacha kuzungumzia mashirikiano mazuri yaliyopo kati ya IPA na UDOM.

Nao baadhi ya watumishi wakieleza changamoto zao wamesema wanakabiliwa na matatizo mbali mbali yakiwemo kutokupata mafunzo ,usafiri ,maslah, na ufinyu wa majengo ya kufanyia kazi .

Close
Close